Nakuru Mbunge Awaanika Wake Zake 2 Katika Hafla Ya Inua Mama

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 13 September 2019.

Hafla ya Inua Mama iliyoandaliwa na seneta Susan Kihika ilikuwa hafla muhimu kwa viongozi wa kike na wabunge wa kaunti ya Nakuru.

Hafla hiyo ilifanyika katika uwanja wa Nakuru ASK, na ilikuwa na wabunge wa kaunti hiyo na viongozi wa kike wanaogemea upande wa naibu rais William Ruto.

Aliwaanika hadharani wake zake wawili, Veronica Wairimu na Dorcas Wangui, huku akiwafichulia kuwa amejifungua hivi maajuzi.

Aliwaambia umati ulikuwa umesisimka, "Huyu hapa ni mmoja wa wake zangu, alijifungua hivi karibuni. Niko sawa ama siko sawa? Inaitwa pekejeng pekejeng pekejeng."

Aliwaalika jukwaani na kumtambulisha mke wa kwanza kwa umati huo, huku akiwafichulia kuwa amejifungua hivi maajuzi.

Aliwaambia umati ulikuwa umesisimka, "Huyu hapa ni Veronica Wairimu, yeye ndiye mke wangu wa kwanza. Na huyu hapa ni Dorcas Wangui, yeye ni mke wangu wa pili. Mke wa tatu hayupo hapa ila mtamleta hapa wakati mwingine. Niko sawa, ama siko sawa? Na, unajua sisaidiangwi....wacha wawe mashahidi wangu. Mimi huwa sisaidiwi, ninauelewa huo mchezo," mwanasiasa huyo aliongeza huku akimregeshea emcee kipaza sauti.

Hafla hiyo ilikuwa na viongozi wa kike wanaogemea upande wa naibu rais William Ruto, ikiwa ni pamoja na seneta Millicent Omanga, mwakilishi wa wanawake kaunti ya Uasin Gishu Gladys Shollei, mwenzake kutoka Bomet Joyce Korir na yule wa Nyandarua Faith Gitau.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...