Skip to main content

Athi River: Sponsa Amfukuza Demu Kikojozi

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 11 September 2019.

Alhamisi, mrembo mmoja wa mtaani wa Athi River alifurushwa na sponsa wake kwa sababu ya kukojoa kitandani.

Penyenye zinaarifu kwamba demu alipatana na buda huyo ambaye inasemekana alikuwa mkwasi wa kutajika akiwa chuo kikuu kimoja cha mjini humo na wawili hao wakaanza uhusiano.

Wapenzi hao walianza kuishi pamoja kama mke na mume hadi wenzake shuleni wakambandika jina la makeke kumaanisha mke wa sonko.

Alhamisi, Taifa Leo ilionyesha kwamba kipusa huyo aliangukia bahati kwani buda alikuwa akimlipia karo ya shule na kukidhi mahitaji yake yote ya chuoni hadi wenzake wakaanza kumuonea kijicho.

Mapenzi ya wawili hao yaliponoga, buda alimnunulia kipusa gari na hata kumkodishia nyumba ya kifahari mtaani humo.

Tabia ya kipusa ilimuudhi sana buda kwa kuwa kando na kuwa mazoea penzi lao lilianza kuingiwa na doa.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →