This archive report was first published on 10 September 2019.
Matumizi ya Kifuu Katika Kuhifadhi Mazingira ¶
Matumizi ya kifuu katika kuhifadhi mazingira ni jambo la kusisimua katika nchi yetu ya Kenya. Kifuu kinaweza kutumika katika mapishi, kutengeneza mafuta ya kujipaka mwilini, kusukia nywele, na kutibu magonjwa kama vile vidonda vya tumbo, kiungulia, na nyoka.
Uzuri wa kutumia kifuu ni kwamba huzuia ukataji miti ovyo na hivyo kuokoa misitu. Serikali imekuwa ikiwekeza mabilioni ya fedha ili kuokoa misitu na kuweka sheria kali za kuzuia ukataji wa miti.
Wakulima wa miti ya minazi wameanzishwa kutumia kifuu badala ya kuni za aina nyingine. Rukia Mtuta, mkaazi wa Taveta, anasema kwamba yeye hatumii kuni za aina nyingine lakini vifuu ambavyo huviokota kwa majirani wanapomaliza kukuna ndunda hilo.
Matumizi ya kifuu pia yamekuwa yakisaidia katika kupunguza rundo za taka zinazotokana na mifuko ya plastiki ambayo ikichomwa husababisha uharibifu wa hewa. Hata baada ya mifuko ya plastiki kupigwa marufuku miaka miwili iliyopita, imekuwa vigumu kupunguza taka za plastiki lakini vifuu vikiendelea kutumika.
Watu wengi hawajui kwamba mkaa wa kifuu ni dawa nzuri wakati wanapokumbwa na magonjwa fulani. Mkaa wa kifuu pia hutumika katika kutengenezea dawa ya mbu na ubani. Vilevile mapambo mengi kwa mfano bangili, herini, mkufu, hutengenezwa kutokana na vifuu.