Skip to main content

Mbunge Alice Wahome: Maisha Yangu Yamo Hatarini Kwa Njama ya Kuua

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 9 September 2019.

Maisha ya Mbunge wa Kandara Alice Wahome yamo hatarini kwa njama ya kuua, alisema Jumatatu, Septemba 9, kwenye runinga ya NTV.

Alisema kuna njama ya kumuua kutokana na msimamo wake wa kisiasa kwenye siasa za 2022, na kwamba mwingine anayelengwa kwenye njama hiyo ni mwenzake wa Kiharu Ndindi Nyoro.

Alidai kuwa kuna mkutano uliofanywa usiku wa manane nyumbani kwa mwanabiashra mmoja mashuhuri Murang'a ambapo njama ya kuwatoa uhai wawili hao ilipangwa.

Waliokuwa wamekusanyika kwenye mkutano huo walikuwa vigogo ambao wanampinga DP Ruto, na kikao cha njama hiyo kilisema kuwa kitamuangamiza Ndindi na hakuna jambo kubwa ambalo litafanyika.

Alisema, "Nina taarifa kuna mkutano ulifanywa nyumbani kwa mfanyibiashra mmoja Kaunti ya Murang'a. Walikuwa wakipanga vile tutaangamizwa."

Aliongeza, "Walisema Ndindi Nyoro ni mtu mdogo na akiuawa, Wakenya watalia na kukashifu serikali kwa muda mfupi tu na kisha kusahau kama ilivyofanyika hapo awali."

Alidai kuwa hayo yote yalihusishwa na siasa za urais za mwaka wa 2022, na kwamba DP Ruto amepata umaarufu mkubwa wa kisiasa na kupata wafuasi wengi.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →