Utata waonekana kuibuka kuhusu ni wapi azikwe Mugabe

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 9 September 2019.

Robert Mugabe, 95, alifariki dunia Ijumaa, Septemba 6, akitibiwa katika hospitali moja nchini Singapore.

Wakati wa kufa kwake, Mugabe alikuwa rais wa zamani wa Zimbabwe, ambaye alitawala nchi hiyo kwa miaka 37 kuanzia 1980 hadi 2017.

Imebainika kuwa kuna utata kuhusu ni wapi azikwe Mugabe, na baadhi ya ndugu zake wanataka azikwe katika kijijini alikozaliwa cha Kutama, yapata kilomita 80 Magharibi mwa mji mkuu Harare.

Wengine wakitaka azikwe katika eneo la makaburi ya Mashujaa lililopo nje kidogo tu ya mji mkuu Harare.

Mpwa wake Mugabe amekanusha madai ya kuwapo mgogoro au suala la kutoelewana na serikali, lakini akakiri kuwa mjomba wake alikufa akiwa mtu mwenye hasira sana baada ya kung'olewa madarakani mwaka 2017 na jeshi pamoja na makamu wake wa zamani.

"Alikuwa mwenye machungu...Unaweza kufikiria watu ambao uliwaamini- watu ambao walikuwa wakikulinda,wakikushughulikia, usalama wako unakugeuka. Alikuwa mwenye masikitiko makubwa na iliweka doa kwenye utawala wake," alisema.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...