Skip to main content

Barcelona Wanamtaka Lionel Messi Kusalia Klabuni Kwa Miaka Iliyosalia Ya Maisha Yake Ya Soka

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 9 September 2019.

Barcelona Wanamtaka Lionel Messi Kusalia Klabuni Kwa Miaka Iliyosalia Ya Maisha Yake Ya Soka

Mkataba wa sasa wa Lionel Messi na Barcelona unakaribia kutamatika katika muda wa miaka miwili, lakini Barcelona tayari wana mipango kuhusu hatma yake.

Kulingana na ripoti za SportsBible, Messi atakabithiwa mkataba mpya na Barcelona ambapo atakamilishia taaluma yake ya soka ugani Nou Camp.

Messi, mshindi huyo mara tano wa Ballon d'Or, amefunga mabao 419 katika mechi 452 za Barcelona, huku akijishindia mataji kadhaa katika kipindi cha miaka 15.

Kuanzia mwaka 2001, Messi alijiunga na Barcelona kupitia kijikaratasi cha nepi, na kuanza taaluma yake ya soka kama mchezaji wa Newell's Old Boys.

Viongozi wa Barcelona wanaamini kuwa Messi, ambaye bado anaendelea kupata nafuu, ni kifaa bora kwa Barcelona, na wanapania kuwa bado raia huyo wa Argentina, ataendelea kuwa na makali yake wakati wa mechi ya Kombe la Dunia la mwaka 2022, itakayoandaliwa nchini Qatar, ambapo atakuwa ametimu wa miaka 35.

Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu anapania kutumia uhusiano wake na babake Messi, kupata saini yake wa mkataba mpya.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →