Wafanyikazi 6 wa G4S wazuiliwa kuhusiana na wizi wa KSh 72M

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 6 September 2019.

Wafanyikazi 6 wa kampuni ya G4S wamezuiliwa kuhusiana na wizi wa KSh 72M uliofanyika Alhamisi, September 5, 2019, katika Kaunti ya Kiambu, Kenya.

Wafanyikazi hao wamefikishwa mbele ya mahakama ya Milimani na kushtakiwa na wizi wa pesa hizo.

Polisi kutoka Kiambu walisema masanduku hayo yalipatikana baada ya mkazi mmoja kuyaona na kufahamisha maafisa wa polisi.

Simu ya rununu pia ilipatikana katika eneo hilo.

Wafanyikazi wa G4S walikuwa wakipeleka fedha hizo kwenye mitambo ya ATM wakati ambapo majambazi waliojifanya maafisa wa polisi waliwafuata na kuponyoka nazo.

Polisi wangali wanachunguza kisa hicho.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...