Robert Mugabe: Dunia yamuomboleza rais wa zamani wa Zimbabwe

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 6 September 2019.

Robert Mugabe: Dunia yamuomboleza rais wa zamani wa Zimbabwe

Robert Mugabe, aliyekuwa rais wa Zimbabwe kwa miaka 37, alifariki Ijumaa, Septemba 6, 2019, baada ya kuugua kwa muda mrefu. Mugabe alitimuliwa mamlakani kufuatia mapinduzi yaliyoongozwa na Emmerson Mnangagwa Novemba 2017.

Alipokuwa mamlakani, Mugabe aliuondoa wadhifa wa Waziri Mkuu na kuwa rais wa nchi hiyo moja kwa moja. Alikuwa Waziri Mkuu wa Zimbabwe 1980 baada ya kushinda uchaguzi wa kwanza kuwahi kufanyika nchini humo.

Itakumbukwa kwamba katika kuhakikisha Zimbabwe inasalia na uhuru wake, Mugabe alimfokea waziri mkuu wa Uingeeza Tony Blair na kumwambia "baki na Uingereza nikiendelea kuichunga Zimbabwe yangu, sihofu vikwazo." Rais huyo wa zamani alianza kuugua mwezi mmoja tu baada ya kutimuliwa mamlakani na kulazwa katika hospitali moja huko Singapore.

Novemba 2018, ilitangazwa kuwa kiongozi huyo amepooza na alikuwa akizuru hospitali mara kwa mara kupokea matibabu.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...