This archive report was first published on 5 September 2019.
Seneta wa Nandi Samson Cherargei amesema zoezi la kufurusha watu kutoka Mau ni mbinu yakummaliza kisiasa William Ruto. Picha: Nation
Alisema zoezi hilo limepangwa na Raila Odinga, na kuwa ni mbinu ya kisiasa kuhakikisha Naibu Rais William Ruto amemalizwa makali yake kufikia 2022 wakati wa mbio za kumrithi Rais Uhuru Kenyatta.
Cherargei alisema wapinzani wa Ruto walileta swala la wanasiasa kuchunguzwa maisha wanayoishi na kisha vita dhidi ya ufisadi.
Waziri wa Mazingira Keriako Tobiko alisema hakuna atakayesazwa kwenye zoezi la kuwafurusha watu kutoka msitu wa Mau.
Alisema serikali imejizatiti kuhifadhi msitu wa Mau na hakuna mtu atasazwa.
Alisema zaidi kuwa zaidi ya familia 10,000 zinatarajiwa kutolewa kwenye msitu wa Mau ikiwa ni zaidi ya watu alfu sitini.