Maafisa wa Raila Odinga Wakabiliana na Maafisa wa Trafiki Nakuru

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 5 September 2019.

Maafisa wa usalama wa Raila Odinga waliagizwa kusimama lakini wakadinda baada ya kufungiwa njia na wanabodaboda walisimama na kutoka wamejihami kwa bunduki.

Maafisa hao walikuwa wamefuatwa na wale wa trafiki kwa madai ya kuendesha gari kwa kasi na kudaiwa kukataa kusimama walipoagizwa kufanya hivyo.

Maafisa wa usalama wa Raila walizua kioja Nakuru baada ya kukataa kusimama walipoagizwa kufanya hivyo na trafiki. Picha: Pristone Mambili

Maafisa hao walipelekwa katika kituo cha polisi cha Central ambapo duru ziliarifu walizungumza na OCPD wa kituo hicho kabla ya simu moja kuingia 'kutoka juu' na kuagiza watano hao kuachiliwa ili waendelee na safari yao.

Maafisa hao walikuwa wanaelekea katika hafla ya ukumbusho wa mwanawe Raila Fidel Odinga, lakini Raila wala jamaa ya familia yake hawakuwa kwenye msafara huo.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...