This archive report was first published on 4 September 2019.
Marriane Kitany na Mithika Linturi walikuwa wakikusanyika kwa mapenzi baada ya kuskizana, alisema mahakama.
Kitany alisimulia hisia zao na kuchora taswira ya usiku wao wa kwanza pamoja kwenye chumba kimoja ndani ya mkahawa wa kifahari wa Sopa Lodge.
Alisema yeye na Linturi waliingia chumba cha kulala baada ya kuskizana, huku wakili wa Linturi akiuliza iwapo mteja wake alihadaiwa kimapenzi.
Kitany alikanusha na kusema hilo lilifanyika baada ya moto wa penzi kuwaka ndani ya wao wawili.
Kitany alisema, "Haikuwa mtego, tulienda kwenye chumba cha mkahawa wa Sopa Lodge baada ya sote kuskizana. Naweza kusema ilikuwa hali ya maskizano kati ya mnunuzi na muuzaji," Kitany alisema huku mahakama ikiangua kicheko.
Kitany na Linturi wana zana mahakamani kwenye kesi ya talaka.