Maafisa wa Sensa Wakuza Mioyo ya Wengi kwa Kumchotea Ajuza Maji Mtoni

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 1 September 2019.

Maafisa wawili wa sensa waliobaki wakijivunia baada ya kumchotea ajuza maji mtoni, kama ilivyotajwa katika picha zilizotolewa kwenye kitandazi cha Facebook.

Wawili hao walionekana wakimsaidia ajuza huyo katika kijiji kimoja kuweza kupata maji huku wakiendesha zoezi la kuhesabu watu.

Maafisa hao wanaonekana kumhesabu ajuza huyo kabla ya kuelekea mtoni na mitungi kumtafutia maji.

Maafisa hao mwanamke na mwanamume, ambao majina yao hayakutambuliwa, waliinama wakachota maji kwa makini kabla ya kurejea nyumbani kwa bikizee.

Bikizee huyo huku akiwa amejaa tabasamu usoni, alikuwa amewasubiri nje ya nyumba yake wawili hao wakiwasali huku wamebeba maji mkononi.

Kama ishara ya shukrani, nyanya huyo aliwaandalia kikombe cha chai na kuketi pamoja nao, kwani wema ulipwa na wema.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...