Skip to main content

Magavana Wachelewa Kuhudhuria Kikao, Wanahabari Waona Kwa Uangalifu

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 31 August 2019.

Magavana waliitishwa kwa wanahabari baada ya kuchelewa kuhudhuria kikao cha habari, na mwanahabari Rose Gakuo aliwataka kuelezea ni kwa nini wamechelewa.

Magavana hao walikutana na hali ambayo hawajazoea baada ya mwanahabari wa runinga kuwazomea kwa kuchelewa kuhudhuria kikao na wanahabari.

Msomaji wa taarifa Rose Gakuo alikerwa na magavana hao baada ya kuwaita wanahabari kwa kikao lakini wakachelewa sana na hivyo kuwaweka kwenye afisi zao wakisubiri.

"Kwa nini hamkufika wakati ambao umeandikwa kikao kilikuwa kianze? Tulikuwa tumefahamishwa tufike 12:30 kama tungeambiwa tuje 2:00pm, basi tungekuja 2:00 pm. Kuambiwa tusubiri kwa masaa mawili unusu si haki kwetu," alisema Gakuo.

Wycliff Oparanya, mwenyekiti wa magavana, alielezea kuwa walikuwa na mabo ambayo yaliwafanya kuchelewesha wanahabari.

"Unajua wakati mwingine kuna masuala mazito ambayo tunafaa kujadili kabla ya kuongea na wanahabari," Oparanya alisema.

Aliomba msamaha kwa wanahabari kwa kuwaweka wakisubiri na ndipo wakaanza kikao.

Magavana hao walikuwa wamekutana kutoa msimamo wao kuhusu swala tata la mgao wa fedha za kaunti.

Walikuwa wakiitaka serikali kuu kutuma fedha zaidi kwenye kaunti huku wakitishia kusitiza shughuli za kaunti kufikia Septemba 16 iwapo hawatakuwa wamepata fedha hizo.

"Kupita tarehe hii, kama swala hili halitakuwa limetatuliwa, basi hatutakuwa na lingine ila kufunga shughuli za serikali za kaunti," alisema.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →