Bungoma: Wachumba walimana makonde baada ya mke kuuza ng'ombe ili ajivinjari Churchil Show ▷ Kenya News

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 30 August 2019.

Bungoma: Wachumba walimana makonde baada ya mke kuuza ng'ombe ili ajivinjari Churchil Show

Wachumba kutoka kaunti ya Bungoma walimana makonde baada ya mke kumuuza ng'ombe apate hela za kuhudhuria Churchil show.

Ng'ombe huyo alikuwa tegemeo kwao kwani alikuwa akiwapa kipato chao cha kila siku, ila alikuwa amemilikiwa na mkewe ambaye alimnunua baada ya kupokea fedha kutoka kwa kikundi cha akina mama miaka miwili iliyopita.

Alhamisi, Agosti 29 jioni, mke huyo alikuwa amewauzia ng'ombe huyo na wakakubaliana amchukue siku itakayofuata asubuhi.

"Nilipigwa na butwaa baada ya kuamshwa na jamaa watatu ambao walidai walikuwa wamekuja kumchukua ng'ombe wao," baba huyo wa watoto watatu alisema.

Ng'ombe huyo alikuwa akiwapa kipato chao cha kila siku, lakini alikuwa amemilikiwa na mkewe ambaye alimnunua baada ya kupokea fedha kutoka kwa kikundi cha akina mama miaka miwili iliyopita.

Wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakijivinjari wakati wa kipindi hicho, na viongozi kutoka Magharibi mwa Kenya wanatarajia kuhudhuria makala hayo.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...