This archive report was first published on 30 August 2019.
Wakati wa kifo cha mwanabodaboda Hassan Mafabi wa Uganda, siri nyingi zilifichuka kuhusu familia yake kubwa.
Alikuwa na wake 6 na watoto 30, na kuacha wajane hao wote wakati wa kifo chake barabarani.
Wengi walishangaa ni vipi mwanabodaboda aliweza kuwalisha wake hao pamoja na watoto 30, ikizingatiwa mapato ya biashara ya bodaboda ni ya wastani tu.
Askofu wa kanisa la Mukono nchini Uganda alidhibitisha kisa hicho na kuwataka marafiki kujitokeza kuisaidia familia ya Mafabi.
Wahudumu wa bodaboda wakisubiri wateja. Picha: Vision
Alisema, 'Tunataka marafiki kujitokeza kuisaidia familia ya Mafabi kwani yeye ndiye alitegemewa kuilisha.'
Alama ya kifo cha Mafabi ilikuwa kwenye ajali ya barabarani, na familia yake inaoboleza baada yake kufariki.
Published on August 30, 2019