Familia ya Nakalira inakabiliwa na hali ngumu baada ya mwili wa jamaa kupotelea katika hifadhi ya maiti

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 30 August 2019.

Familia ya Nakalira inakabiliwa na hali ngumu

Mary Sakaria aliaga dunia Agosti 14, 2019, na mwili wake ukahifadhiwa mochuari ya Hospitali ya Dreamland mjini Kimilili wakati familia ikiandaa mazishi.

Walipokuwa wakijaribu kuuchukua mwili Jumatatu, Agosti 26, iligunduliwa kuwa mwili ulikuwa umepewa familia nyingine.

Wasimamizi wa mochuari hiyo waliitaja kuwa mwili ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Lugulu na baadaye kuzikwa Sirisia, Ijumaa Agosti 23.

Longinus Wekesa mjomba wa Mary Sakaria alisema, "Tumegundua mwili wa mpwa wangu ulichukuliwa na familia nyingine na kupelekwa katika Hifadhi ya Hospitali ya Lugulu kisha ukapelekwa Ndakaru, Bungoma Magharibi kuzikwa."

Spika wa Seneti Ken Lusaka, Gavana wa Bungoma Wycliffe Wangamati, na Mbunge wa Sirisia John Waluke walihudhuriwa kwenye mazishi ya Sirisia.

Wekesa aliongeza, "Walishtuka kupata kuwa walizika mwili usiokuwa wa jamaa yao hata baada ya kutumia zaidi ya KSh 2 milioni kuandaa mazishi."

Shughuli za kufukua miili ya wawili hao inaendelea ili kila familia kuzika mwili wao na kesi tayari imepelekwa katika Kituo cha Polisi cha Kimilili.

Familia zikitaka hifadhi ya maiti kughirimia gharama zote, pia kumepangiwa kufanyiwa tamiko ili kuondoa laana kwa mujibu wa mila na desturi za jamii ya Wabukusu.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...