Skip to main content

Kenya: Serikali Yafunga Shule 15 Kwenye Msitu wa Mau Huku Ikifurusha Walio Ndihi

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 29 August 2019.

Kenya: Serikali Yafunga Shule 15 Kwenye Msitu wa Mau Huku Ikifurusha Walio Ndihi

Serikali ya Kenya imefunga shule 15 kwenye msitu wa Mau huku ikifurusha walio ndani ya msitu huo. Hii ni kufuatia kudaiwa kwamba watu wanaonyakua sehemu ya msitu huo.

Shule hizo zimefungwa kwa sababu serikali inasema kuwa ujenzi wa shule hizo ulifanyika kinyume cha sheria. Serikali inaendesha zoezi la kuwafurusha walio ndani ya msitu huo.

George Natembeya, mshirikishi wa eneo la bonde la ufa, alisema kuwa shule hizo hazikuwa zimesajiliwa kwa sababu hazina stakabadhi zozote kwa kuwa ziko kwenye msitu. Pia alisema kuwa shule hizo hazina wanafunzi wanaotarajiwa kukalia mtihani wa kitaifa mwaka huu.

Shule hizo ni: Kirobon Centre, Senetwet Centre, Kapsilibwo Centre, Kitoben Centre, Indianit Centre, Kabarak Centre, Noosagami Centre, Chorwet Centre, Ogilge Centre, Sebetet Centre, Olabai Centre, Koitabai Centre, Chebirbelek Centre, Chebetet Centre, na Lelechwet Centre.

Maafisa wa polisi pamoja na wanahabari wafuatilia uharibifu kwenye msitu wa Mau. Zoezi hilo litawaacha watu wa familia 10,000 kwenye hatari ya kufurushwa makao.

Source: Tuko, 2019-08-29T10:17:04.000Z

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →