This archive report was first published on 28 August 2019.
Seremala Alikatwa na Msumeno wa Umeme, Madaktari Waliunganisha Mkono Wake ¶
Anthony Lelliott, seremala mwenye umri wa miaka 46, alikata bodi ya sakafu na kuuwacha mkono wake ukining'inia kati ya ngozi na mfupa. Hii ilikuwa baada ya ajali hiyo wakati alipokuwa anakata bodi ya sakafu akitumia mashine hiyo yenye nguvu.
Madaktari walimfanyia upasuaji wa kuunganisha mkono huo kwa takriban saa 17 katika hospitali ya Mt. George London. Upasuaji huo ulikuwa wa kuunganisha mfupa uliokatika na vile vile mishipa ya damu.
Wataalamu wa upasuaji walikuwa na imani kwamba mkono wa Lelliott ungekunjika na kuguza kitu, hata hivyo, madaktari hao walikuwa na kibarua sio tu kuunganisha mkono bali pia mfupa uliokatika na vile vile mishipa ya kusukuma damu.
Anthony Lelliott alisema hakufahamu jinsi mkono wake ulivyofikia msumeno ila aliona damu nyingi ikitapakaa kwenye sakafu. Lelliott alielezea kufurahishwa na huduma na juhudi zilizofanywa na madaktari hao kuhakikisha hali yake inarejea kawaida.
"Ninashukuru kila mmoja aliyenihudumia, maneno hayawezi eleza furaha yangu kwa sababu nungekuwa naamka kila siku bila mkono wangu mmoja. Kwa sasa ninajaribu tu kuzoea namna ya kuutumia, ninashukuru sana". Lelliott alisema.