Skip to main content

Waiguru: Mt Kenya Tunaunga Mkono BBI

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 28 August 2019.

Gavana wa Kirinyaga Anne Mumbi Waiguru amesema eneo la Mlima Kenya linaunga mkono timu ya BBI iliundwa na Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga kuchukua maoni kuhusu mabadiliko yanayohitajika kwenye uongozi wa Kenya.

Waiguru alisema eneo hilo linasubiri mapendekezo ya BBI huku akishabikia kukataliwa kwa mswada wa Punguza Mzigo unaopendekewa na Ekuru Aukot katika bunge la kaunti ya Nyeri.

Waiguru alisema, "Kama nilivyosema awali, Mt Kenya inaunga mkono BBI na hilo limeonekana leo baada ya mswada uliopendekezwa na Ekuru Aukot kuangushwa na bunge la Nyeri."

Alisema pia kuwa yale yaliyotokea kwenye bunge la Nyeri ni ishara ya mambo yatakavyokuwa kwenye kaunti zingine za Mlima Kenya.

Waiguru aliwataka viongozi wote wa Mlima Kenya kuunga mkono urafiki kati ya Raila Odinga na Uhuru Kenyatta, akisema kuwa Uhuru atasalia kuongoza jamii za Mlima Kenya kisiasa.

Alisema hakuna mwanya wa uongozi kwenye eneo hilo na hivyo viongozi wanafaa kumfuata Kenyatta.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →