This archive report was first published on 26 August 2019.
Maafisa wa sensa wapatao 70 wa Kilifi Kusini, Kaunti ya Kilifi waliripotiwa kususia kazi baada ya kudai malipo ya marupurupu ya kushiriki zoezi la mafunzo kuhusu sensa Jumatatu, Agosti 26.
Maafisa hao waligoma kuendelea na kazi 4pm na kufanya maandamano barabarani, kwa mujibu wa ripoti ya K24.
Maafisa hao walidai zaidi ya KSh 2,000 pesa za marupurupu ya kushiriki zoezi la mafunzo kuhusu kuhesabu watu, walizofaa kulipwa kabla ya zoezi hilo kuanza rasmi.
Ingawa hiki ni kisa cha kwanza tangu zoezi hilo kuanza rasmi Jumamosi, Agosti 24, maafisa hao walisema walisusia kazi baada ya kupata habari kuwa, wenzao katika maeneo mengine walikuwa wamelipwa tayari.
Maafisa hao walisema walisusia kazi baada ya kupata habari kuwa, wenzao katika maeneo mengine walikuwa wamelipwa tayari.