Mwanga wa Kiswahili: Mazoea Mabaya Katika Kiswahili

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 26 August 2019.

Makosa ya Mazoea Katika Kiswahili

Leo, tutakapofika, tutazidi kuangaza makosa ya mazoea katika matumizi ya lugha ya Kiswahili. Katika makala yetu ambayo yamepita, tumekuwa tukiweka mwanga katika Kiswahili na kuinyoosha lugha. Published on August 26, 2019

Leo, tutazidi kuona na kunyoosha palipo na utata. Picha: UGC

Makosa: Chakula Chenye Tulikula Kilikuwa Hakijaiva

Neno "chakula" limetumika visivyo. Sahihi: Chakula ambacho tulikula kilikuwa hakijaiva au Chakula tulichokula kilikuwa hakijaiva.

Makosa: Viongozi Wenye Tulichagua Ni Fisadi

Sahihi: Viongozi ambao tulichagua ni fisadi au Viongozi tuliowachagua ni fisadi.

Makosa: Gari Lenye Amenunua Ni Nzuri Sana

Sahihi: Gari ambalo amenunua ni zuri sana au Gari alililonunua ni zuri sana.

Makosa: Hakuna Binadamu Hapendi Maendeleo

Sahihi: Hakuna binadamu asiyependa maendeleo.

Makosa: Wanafunzi Wenye Walikalia Mtihani Mwaka Jana Walipasi Vizuri

Sahihi: Wanafunzi ambao walifanya mtihani mwaka jana walipasi vizuri au Wanafunzi waliofanya mtihani mwaka jana walipasi vizuri.

Makosa: Mtoto Yule Ni Mrefu Kuwaliko Wazazi Wake

Sahihi: Mtoto yule ni mrefu kuliko wazazi wake.

Makosa: Mtoto Yule Ni Mnene Kumliko Wake

Sahihi: Mtoto yule ni mnene kuliko wake.

Wakati unapotumia "o" rejeshi huwezi kutumia pamoja na kirejeshi amba. Mfano zaidi ya makosa haya ni;

Makosa: Mtu Ambaye Aliyekuja Alikuwa Mgeni Wetu

Sahihi: Mtu ambaye alikuja alikuwa mgeni wetu au Mtu aliyekuja alikuwa mgeni wetu.

Kumbuka Kiswahili ndio fimbo ya Mwafrika tuitumie.

Makala haya yameandikwa na Sakwa Titus mwalimu, mhakiki na mwandishi.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...