This archive report was first published on 24 August 2019.
Wachawi waonywa dhidi ya kutatiza zoezi la sensa ¶
Wachawi wa kukimbia usiku Kaunti ya Homa Bay wametakiwa kufunga biashara yao kwa siku mbili ili kuruhusu zoezi la sensa kufanyika bila ya kutatizwa.
Harman Shambi, Kamishna wa Kaunti ya Homa Bay, amewataka wachawi kujizuia kutoka usiku ili nao pia wahesabiwe.
Shambi alisema, "Ni Wakenya na hivyo ni lazima kuhesabiwa. Kwa hivyo ni lazima kujizuia kutoka usiku ili wahesabiwe," kwa mujibu wa Nation, Jumamosi, Agosti 24, 2019.
Ujumbe huo ulifuatia ujumbe wa Twitter uliotamba sana wiki hii uliodai Waziri wa Usalama wa Ndani Dk Fred Matiangi amepiga marufuku shughuli za wachawi wote wa usiku kaunti za Homa Bay na Kisii wakati wa sensa.
Shambi pia aliwataka watu wanaopanga kujifanya ni maafisa wa sensa ili kuwahangaisha watu kwamba, watachukuliwa hatua kali za kisheria, aliwataka raia kuwa makini na kuchukua tahadhari za mapema.
Shambi alisema, "Maafisa wa sensa watajitambulisha na watachomoa baji zao ma jaketi zao za kumwe kwenye mwangaza. Wataandamana na machifu na wazee wa vijiji ili kuifanya kazi hiyo kuwa rahisi,".
Shughuli za wachawi katika maeneo mengi ya humu nchini hufanywa usiku, na sarakasi zao huwa ni za kutisha mno; miongoni mwazo ni kutimka mbio na kuramia miti katika maboma ya watu, kurusha mawe na mchanga kwenye paa na ndani ya nyumba, kuacha vinyesi katika maboma ya walengwa wao miongoni mwa nyinginezo nyingi.
Shughuli za wachawi katika maeneo mengi ya humu nchini hufanywa usiku, na sarakasi zao huwa ni za kutisha mno.
Shughuli za wachawi katika maeneo mengi ya humu nchini hufanywa usiku, na sarakasi zao huwa ni za kutisha mno.