Skip to main content

TSC na KUPPET Wakubaliana Kutangaza Nafasi za Kazi kwa Walimu Wenye Diploma

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 23 August 2019.

Walimu 38,000 wenye diploma watakuwa na fursa ya kuwania vyeo kuanzia Jumanne, Agosti 27, baada ya TSC na KUPPET kufikiana.

TSC itafanya uamuzi kuhusu idadi ya walimu ambao watapandishwa cheo kati ya walimu 38,000 wakizingatia muda wa kuhudumu, nafasi za kazi zilizopo na kiwango cha masomo.

Maafisa wa KUPPET na TSC walikuwa na kikao mnamo Agosti 22, 2019, jijini Nairobi, ambapo walikubaliana kutangaza nafasi za kazi ifikiapo Jumanne, Agosti 27.

Walimu wote wenye diploma wataruhusiwa kutuma maombi ya nafasi hizo ambazo zitakuwa kutoka kikundi cha Job Group C2 hadi C3.

Wanafunzi wanaohudumu chini ya tume ya KNUT watakosa nafasi za kupandishwa cheo.

Maafisa wa KUPPET walipendekeza kuongezwa kwa mshahara wa walimu hadi asilimia 70.

Maafisa wa TSC walipendekeza kuwapa marupurupu walimu wanaohudumu katika shule za upili.

Maafisa wa KUPPET walipendekeza kuwapa marupurupu walimu wanaohudumu katika shule za upili.

Walimu ambao wanahudumu katika viwango vya Job Group (Grade C) na Job Group J (Grade C1) hawakujumuishwa katika mpango wa kupandishwa cheo kulingana na mkataba wa makubaliano ya CBA 2017-2021 uliyotakiwa kuanza Julai 1, 2019.

Aidha mapema juma hili, TSC ilitangaza itawapadisha vyeo takriban walimu 6,043 wanaohudumu katika viwango vya Grade C5 na C4 na kuwapa nafasi ya kuwa walimu wakuu na manaibu walimu wakuu.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →