Tabitha Karanja aachiliwa kwa dhamana ya KSh15 milioni baada ya kukanusha mashtaka

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 23 August 2019.

Tabitha Karanja aachiliwa kwa dhamana ya KSh15 milioni baada ya kukanusha mashtaka

Agosti 23, 2019

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Keroche, Tabitha Karanja, aachiliwa kwa dhamana ya KSh15 milioni baada ya kukanusha mashtaka ya kukwepa kulipa ushuru wa KSh14 bilioni.

Uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mkuu Francis Andayi, ambaye alimkabithi Tabitha masharti hafifu kwa sababu ya hali yake ya kiafya.

Andayi alisema, "Ninamuzuia kuingia korokoroni na kisha kufariki akiwa huko na kulaumu mahakama," kwa hivyo kuagiza Tabitha kuzilipa pesa hizo katika kipindi cha siku saba la sivyo wakuregenzi wote watakamatwa isipokuwa mshtakiwa wa pili.

Tabitha anatazamiwa kuafikiana na masharti hayo kabla ya siku kuisha.

Washukiwa hao wameshtakiwa kwa mashtaka ya kukwepa kulipa ushuru cha kiasi cha KSh14 bilioni.

Uamuzi huo ulitolewa siku ya Ijumaa, Agosti 23, 2019.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...