Skip to main content

Gavana Ferdinand Waititu Akiri Kuogopa Waziri Fred Matiang'i

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 23 August 2019.

August 23, 2019: Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu amekiri kuogopa sana Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i.

Waititu alipokuwa akizungumza baada ya kuhudhuria misa ya ukumbusho wa hayati Mzee Jomo Kenyatta, iliyoandaliwa katika Kanisa Katoliki la Holy Family Basilica, Nairobi, alikiri anamuogopa pia seneta mteule Maina Kamanda.

Video iliyosambazwa sana mitandaoni inaonyesha Waititu akiang'ua kicheko pamoja na Naibu Rais William Ruto, Maseneta Kipchumba Murkomen, Johnson Sakaja, Kiongozi wa Wengi Bunge la Kitaifa Aden Duale, na Seneta Mteule Maina Kamanda.

Waititu alisema, "Wacha niwambie ukweli wale ambao wananilemea sana ni Matiang'i na Maina Kamanda...Njoro siku hizi hakutani na Matiang'i. Lakini mimi ni mtu wa Mungu," alisema Waititu.

Waititu amekuwa akikumbwa na masaibu chungu mzima baada ya kutuhumiwa kwa ufisadi akiwa pamoja na mkewe Susan.

Wawili hao walikuwa miongoni mwa washukiwa 11 ambao wanatuhumiwa na madai ya ubadhirifu wa KSh 588, 198, 328 za zabuni ya ujenzi wa barabara na zingine zilizokuwa zimetengewa kuendesha shughuli za kaunti hiyo.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →