Mama Fua wa Kiambu atumia Twitter kupiga upato kazi yake

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 22 August 2019.

Wakati wa kila mtu anapiga upato kazi yake kwa njia ya kawaida, mama Lucy Wanjiru wa Kiambu, ambaye anatoka Uthiru, amekuwa kutumia mtandao wa Twitter kupiga upato kazi yake ya kufua.

Alisema alikutana na rafiki yake mmoja wa shule ya upili na kumfungua macho ya jinsi anaweza kutumia mitandao kutangaza kazi yake.

"Sikujua kuhusu Twitter, lakini siku moja rafiki yangu akaniambia kuihusu. Alinifungulia akaunti lakini sikujua ni itumie vipi. Ndipo akanielezea vile inatumika na jinsi naweza kuitumia kutangaza kazi yangu," alisema.

Wanjiru alielezea kikosi cha TUKO.co.ke jinsi ambavyo baadhi ya watu walimkataza kuchapisha kazi yake mitandaoni wakisema ni ya kiwango cha chini.

"Baadhi ya watu walisema sifai kuchapisha kazi yangu wakidai ni ya aibu na nafaa angalau kuulizia kazi ya kuosha afisi ama kupika chai," aliongeza.

Alipata wateja wawili ambao baadaye walimpendekeza kwa marafiki zake.

Wanjiru amewataka wote wanaotafuta kazi wasichague kazi yoyote.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...