This archive report was first published on 22 August 2019.
Mwili wa Mzee Kenyatta: Mwanaharakati Boniface Mwangi Ameitaka Serikali Kuwasafirisha Kwaajili ya Kumbukumbu ¶
Wakati wa kusherehekea kumbukumbu za Mzee Jomo Kenyatta, mwanaharakati wa haki za binadamu Boniface Mwangi ameitaka serikali kuyasafirisha mabaki ya hayati Mzee Jomo Kenyatta kutoka majengo ya Bunge hadi katika makazi yake ya eneo la Gatundu, kaunti ya Kiambu.
Alisema wakati wa kuundoa mwili huo jijini umewadia ndiposa wananchi waweze kupona makovu aliyowasababishia wakati wa utawala wake.
Aliongeza kwamba, rais huyo wa kwanza wa nchi alipanda mbegu ya ufisadi na hata kuweka mikakati ambayo imemfanya mwanawe, Uhuru Kenyatta, kuliongoza taifa.
Alisema Mzee Kenyatta alikuwa muuaji, mwizi, na alileta ukabila, na kuwaida familia yake kushiriki uwindaji haramu wa ndovu wetu.
Aliongeza kwamba, rais huyo wa kwanza wa nchi alipanda mbegu ya ufisadi na hata kuweka mikakati ambayo imemfanya mwanawe, Uhuru Kenyatta, kuliongoza taifa.
Alisema janga la umaskini ambalo limeikumba nchi lilisababishwa na utawala mbaya wa hayati.
Wakili Miguna Miguna alisema walipa ushuru wanapaswa kurejeshewa fedha ambazo zimetumika katika kulihifadhi eneo alikozikwa.
Alisema hii ni wakati taifa linaposherehekea kumbukumbu za Mzee Kenyatta ambaye alifariki mnamo Agosti 22, 1978 akiwa katika likizo mjini Mombasa.