Waziri Matiang'i Aomba Radhi Kwa Kufungwa Kwa Baa Kwa Ajili Ya Sensa 2019

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 22 August 2019.

Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i ameshikilia kwamba maeneo yote ya burudani yatafungwa baada ya saa kumi na moja jioni kufuatia sensa ya 2019 ambayo inang'oa nanga Jumamosi, Agosti 24.

Alipohutubia waandishi wa habari katika jengo la Harambee Alhamisi, Agosti 22, Matiang'i hata hivyo, aliomba radhi kwa kutoa amri hiyo na kuwataka wapenzi wa mvinyo kuburudika mchana.

Alisema kuwa zoezi la kuhesabu watu hufanyika mara moja baada ya miaka 10 na kwamba aliamuru maeneo yote ya burudani kufungwa kuanzia saa kumi na moja jioni.

Aliongeza kuwa shughuli zinazoendelea Jumapili na Jumamosi majira ya usiku haziwaathiri tu wale ambao watakuwa katika maeneo ya burudani.

Alisema kuwa aliamuru muelekee nyumbani ifikiapo saa kumi na moja jioni ili muhesabiwe.

Shughuli ya kuhesabu watu itang'oa nanga Agosti, Jumamosi 24 usiku na kukamilika Agosti 31.

Wakati wa zoezi hilo kila mtu atahesabiwa kulingana na mahali atakapokuwa wakiwemo wasafiri, wale watakaokuwa mahotelini na katika taasisi zote nchini.

Kenya imo miongoni mwa nchi chache ambazo hushiriki zoezi la kuhesabu watu kila baada ya miaka 10.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...