Skip to main content

Seneta Mithika Linturi na Mary Keitany: Kesi ya Talaka Imefichua Wandani wa Ruto na Uhuru

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 20 August 2019.

Seneta wa Meru Mithika Linturi na aliyekuwa mkuu wa wafanyikazi katika afisi ya Naibu Rais William Ruto, Mary Keitany, wanaogopa kuhukumiwa kwa kesi ya talaka yao, kwa kuwa imefichua jinsi wandani wa Ruto na wa Rais Uhuru Kenyatta walipanga kumuokoa aliyekuwa waziri wa Ugatuzi Ann Waiguru asing'atuliwe mamlakani.

Waiguru alikuwa waziri wa kwanza wa Ugatuzi ndani ya serikali ya Jubilee baada ya Ruto na Uhuru kupata ushindi wa urais mwaka wa 2013.

Keitany alisimulia mahakama jinsi ambavyo mapenzi yao yalianza na baadaye kushika kasi. Alisema kwamba penzi lao lilishika motokatika chumba kimoja cha kulala katika mkahawa mmoja wa kifahari Naivasha ambapo wawili hao walilala na kufurahia penzi usiku kucha.

Keitany alisema siku ambapo Linturi alitarajiwa kuwasilisha mswada bungeni wa kumng'atua Waziri Waiguru, kuhusiana na wizi wa mamilioni ya pesa katika NYS, njama ilipangwa na wandani wa vigogo hao wawili wa Jubilee na ndipo seneta huyo akapangiwa safari ya mapenzi pamoja naye huko Naivasha.

Keitany alisema hapo ndipo kaa la penzi lao liliwaka moto na wakaanza kuwa wapenzi.

Keitany anapinga madai ya Linturi kuwa alikuwa anaishi kwake kama mgeni tu na wala wawili hao hawakuwa wameoana wala kuwa na uchumba.

Keitany alisema kwamba Linturi alimjulisha kwa watoto wake na akaanza kuwashughulikia kama mama yao.

Keitany alisema kwamba Linturi alikuwa na chumba cha kulala kwa siku kadhaa kabla ya baadaye kuanza kuishi na mimi Kileleshwa.

Kesi hiyo itaendelea Jumatano, Agosti 21.

Be the first to react

Follow the next update

Build Nyakundi Report with us

Join the official channels for story updates, video drops, and alerts from the newsroom. Call 0710 280 973.

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →