Mbunge wa Zamani wa Kasarani Elizabeth Ongoro Ameamini Kuendelea na Uchaguzi Kibra

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 17 August 2019.

Mbunge wa zamani wa Kasarani Elizabeth Ongoro amesema kuwa atakuwa tayari kuchukua kiti cha ubunge eneo la Kibra baada ya kifo cha mbunge Ken Okoth.

Aliwaomba Wakenya kuendelea kuweka amani kote nchini na kuonyesha mfano mwema wanavyofanya Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa Upinzani Raila Odinga.

"Nashukuru sana kwa viongozi wetu wawili kwa kutuonyesha njia, kwa kuwa Ukristo ni Amani, Mapenzi, Umoja na kuishi pamoja kwa utangamano" Ongoro alisema.

Notisi ya Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi kwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati iliipa tume nafasi ya kuanza matayarisho na kupanga tarehe ya uchaguzi mdogo ambao ni lazima kufanyika katika kipindi cha siku 90 kwa mujibu wa Katiba.

Wengine waliokuwa wakidaiwa watashiriki ni Katibu Mkuu wa Orange Democratic Movement (ODM), Edwin Sifuna, Sigar James Agumba na kiongozi wa Vijana ODM Benson Musungu.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...