Skip to main content

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi Aunga Mkono Mswada wa Punguza Mizigo

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 16 August 2019.

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi Aunga Mkono Mswada wa Punguza Mizigo

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi ameunga mkono mswada wa Punguza Mizigo, akisema kwamba mapendekezo yaliyomo ni suluhu kwa matatizo yanayowakumba Wakenya.

Alitoa wito kwa wanasiasa wengine kumuunga mkono mswada huo, akisema kwamba itawasaidia Wakenya kupata huduma bora.

Alisema hivi wakati wa kuwasilisha taarifa kwa wakazi wa kaunti ya Turkana mnamo Alhamisi, Agosti 15, 2019, wakati wa hafla iliyohuduriwa na Naibu Rais William Ruto.

Alisema kwamba kura ya maamuzi ambayo inawadia ni ile ya Punguza Mizigo pekee, na kwamba watafeli katika juhudi za viongozi wengine wanaounga mkono rais Uhuru Kenyatta na kinara wa upinzani Raila Odinga katika kura ya maamuzi chini ya jopo kazi la Building Bridges Initiative (BBI).

Naibu Rais William Ruto alikwepa kuzungumzia suala hilo katika hotuba yake, lakini amekuwa akiyarai makundi yote mawili ambayo yamekuwa yakilipigia debe suala la katiba kufanyiwa marekebisho kujiunga pamoja na kuwapa nafasi Wakenya kujifanyia uamuzi wenyewe.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →