This archive report was first published on 15 August 2019.
Ali Punjani, mshukiwa wa ulanguzi wa dawa za kulevya, alitumia mamilioni ya fedha kugharamia kampeni za wawaniaji wawili wa urais pamoja na magavana wawili, kulingana na taarifa kutoka kwa makachero wanaomchunguza uuzaji wa madawa ya kulevya mjini Mombasa.
Polisi walipoingia nyumbani kwa Punjani kufanya msako siku ya Jumanne, Agosti 13, walikuta alitumia pesa kwa ajili ya kampeni za wanasiasa, kwa pamoja na MaMCAs na Wabunge kadhaa.
Ali Punjani, ambaye kwa sasa anapokea matibabu nchini India, anahusishwa na ulanguzi wa mihandarati baada ya kudaiwa kuwa rafiki wa karibu wa familia ya Akasha.
Watoto wawili wa familia ya Akasha wanakabiliwa na mashtaka nchini Marekani ya uuzaji madawa ya kulevya na walikubali mashtaka hayo.
Maafisa wa polisi walipiga nyumbani kwake msako, na hatua hiyo ilihakikisha kuwa taarifa kuhusu uhusiano wa Punjani na wanasiasa ilifichuka.