This archive report was first published on 15 August 2019.
Wanamuziki wa Kenya wamezuka kwa hasira na kulisuta shirika la muziki la Music Copyright Society of Kenya (MCSK) baada ya kuwalipa pesa za chini.
Wanamuziki hao walilipwa KSh 2530, ambayo ni ada ya kuzitoa, na hata hivyo, hatua hiyo ya MCSK kuwalipa baada ya kuzikusanya pesa kwa miezi miwili haikupokelewa vyema.
Wanamuziki hao walisema kuwa walikuwa wamechezewa shere na kuwa walilazimika kufanya kazi bila malipo ya kutosha.
Msanii wa injili Willy Paul alisema kuwa pesa zinazotumika kutengeneza muziki ni nyingi na hivyo wasanii wanastahili kupokea malipo yanayofaa.
Alisema, "Hizi doh (pesa) mnatumia watu ni za nini? Ni za credit (malipo ya maongezi ya simu) ama nini? …nyambeni huko, sawa, nyambeni huko…"