Gavana Mike Sonko Akataa Ombi la Kazi la Jamaa Mmoja

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 14 August 2019.

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amekataa ombi la kazi la Philip Sogoti Chepsat, ambaye aliongoza ombi lake kupitia gazeti la Tuko.co.ke.

Ujumbe uliochapishwa Facebook mnamo Jumatano, Agosti 14, 2019, Sonko alimuarifu Chepsat kwamba ombi lake halikufaulu kwa sababu hakuwa mwanamke, ambayo ilikuwa ni kipengele muhimu cha ahadi yake ya kuwahudumia wanawake katika uongozi.

"Kama mwanasisasa, wajibu wangu ni kuwatimizia wananchi walionipigia kura ahadi yao. Na kutokana na hilo, niliwaahidi wakazi wa Nairobi kwamba wadhifa huo wa naibu gavana nitawatengea wanawake. Samahani kwa kuwa wewe sio mwanamke. Nanuia kuwatimizia ahadi wanawake kwa kuwa lazima kuwepo na usawa katika uongozi. Hii ndio maana nusu ya wanachama wanaohudumu katika kaunti ya Nairobi ni wanawake," alisema Sonko.

Aliukosoa wasifu wa Chepsat na kusema kwamba ni vyema angeeleza kwa kina kuhusu uzoefu wake wa kazi ndiposa serikali ya kaunti ingefanya maamuzi kuhusu nafasi ya kazi ambayo ingemfaa na kuweza kumsaidia siku za usoni.

"Nakuomba kwamba usikate tamaa maishani wakati unapojikaza kuafiki ndoto yako ya kuwahudumia wakazi wa kaunti ya Nairobi. Endelea kufuatilia nafasi za kazi zinazotangazwa na kutuma maombi....hata hivyo nakutakia kila la heri wakati ukiendelea katika shughuli zako za kila siku kama mkaazi wa Nairobi," alisema Sonko.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...