This archive report was first published on 14 August 2019.
Sheria ya Kuwapiga Teke Magavana: Kesi za Uhalifu wa Kiuchumi ¶
Mabadiliko yaliyofanyiwa Tume ya Kupambana na Uhalifu wa Kiuchumi nchini Kenya na kitengo cha Jinai kinachoshughulikia maswala ya uhalifu wa kiuchumi vimeinua imani ya wakenya na ari yao ya kusaka haki.
Ukosefu wa ushahidi na mashahidi kukosa kuwasilisha ushahidi wao mbele ya hakimu ni jambo la kawaida kila kuchao. Jambo hili limewafanya wakenya wengi kupoteza matumaini ya kupata haki mahakamani kwa kesi zinazowahusisha viongozi wa ngazi za juu serikalini na katika ngazi ya Kaunti.
Imani ya wakenya inaendelea kuboreshwa kwa uwezo wa Tume ya Kupambana na Uhalifu wa Kiuchumi na kitengo cha Jinai kinachoshughulikia maswala ya uhalifu wa kiuchumi kushughulikia maswala ya uhalifu wa kiuchumi. Hata hivyo, kuimarishwa kwa taasisi hizo imekuwa tisho kubwa kwa uongozi wa Magavana kwani hadi sasa Magavana ambao hawajawajibika kikamilifu katika serikali zao wana kila sababu ya kuwa na wasi wasi kwani endapo kutakuwapo ushahidi wa kuyapa nguvu madai ya matumizi mabaya ya mamlaka watatakiwa kuondoka mamlakani na kusubiri kujua hatima yao nje ya a? si zao.
Magavana wengine wenye kesi za uhalifu wa kiuchumi dhidi yao ni pamoja na Gavana wa Samburu Bwana Moses Kasaine Lenolkulal ambaye sawa na mwenzake wa Kiambu amezuiliwa kuendelea kutekeleza majukumu yake hadi kesi dhidi yake kusikilizwa na kuamuliwa.
Wakosa usingizi Hatua ya mahakama kutoa agizo la kuzuiliwa kwa wawili hawa na mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Bwana Nurdin Haji kutaka kesi ndhidi ya Gavana wa Busia Bwana Sospeter Odeke Ojamong kutadhminiwa upya na kuamuliwa kama anastahili kuwa A? sini huku kesi yake kuhusu ubadhirifu wa fedha.
Magavana na kaunti zinginezo zinazopigwa Kurunzi na tume ya uhalifu wa kiuchumi - EACC ni pamoja na Mohamed Ali wa Marsabit, Muthomi Njuki wa Tharaka Nithi, Mwangi wa Iria wa Murang’a, Charity Ngilu wa Kitui na Granton Samboja wa Taita Taveta Mwenyekiti wa Baraza la Magavana aliye pia Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya amewahimiza wanasheria barazani humo kuchunguza iwapo ipo nafasi ya kisheria na kwa kuzingatia haki za kibinadamu kuwaruhusu magavana wenzake kusalia mamlakani wanapoendelea kujibu mashtaka ya uhalifu wa kiuchumi dhidi yao.