Familia ya Marehemu Mbunge wa Kibra Ken Okoth Kwa Kukataa KSh 32 Milioni

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 14 August 2019.

Familia ya Marehemu Mbunge wa Kibra Ken Okoth Kwa Kukataa KSh 32 Milioni

Familia ya marehemu Mbunge wa Kibra Ken Okoth inatazamia kupokea KSh 32 milioni kutoka bunge, ikiwa ni sehemu ya pesa za bima na malipo ya kifo.

Kufikia sasa, familia bado haijasema ni nani wa kuachiwa jukumu la kusimamia nyumba za marehemu.

Bunge linatazamiwa kutoa pesa hizo mara korti ikiamua ni nani anayefaa kusimamia mali ya marehemu Ken Okoth.

Kwa mujibu wa sheria ya Malipo ya Uzeeni ya Bunge, wabunge waliohudumu mihula miwili na zaidi tu wanaofaa kupokea malipo ya takrian KSh 125,000 kila mwezi hadi kifo.

Wanaohudumu muhula mmoja tu huregeshewa michango yao na 15% ya pesa hizo kila mwaka.

Karibuni, Kiongozi wa Wachache Bungeni John Mbadi alipendekeza kufanyiwe marekebisho sheria hiyo ili wabunge waliostaafu kati ya 1984 na 2001 wanalipwa KSh 100,000 kila mwezi hadi kifo.

Imran, kaka ya marehemu Okoth, alisema kuwa suala hilo ni la kifamilia na linashughulikiwa na wakili.

Imran alisema, "Sijui nani anawapa hizi taarifa zote na kutaja kiasi cha pesa. Kwa nini afanye hivyo wakati hiki ni kitu kinachofaa kuwa siri?"

Familia ya marehemu inatazamia kupokea KSh 32 milioni kutoka bunge, ikiwa ni sehemu ya pesa za bima na malipo ya kifo.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...