Wendy Waeni: Mamake ni Mlevi, Joe Mwangi Adai

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 13 August 2019.

Wendy Waeni, mwanasarakasi maarufu, amekuwa katika mizozo na meneja wake Joe Mwangi kuhusu matumizi ya fedha za mtoto wake.

Joe Mwangi, meneja wa Wendy Waeni, amejitokeza kusema kuwa mamake Wendy ni mlevi na hivyo amekuwa akitumia fedha za mtoto wake vibaya.

Alidai kuwa kwa wakati mmoja alilazimika kutoa fedha zake mwenyewe kugharamia masomo ya mwanasarakasi huyo lakini mamake akazifyonza.

"Mwezi Disemba, nililazimika kutoa pesa zangu shilingi 100, 000 nikapatia mamake kwa sababu Wendy alikuwa aingie shule Januari. Kufikia shule kufunguliwa, alikuwa hana pesa hizo na Wendy alianza kunitumia jumbe akiniuliza kwani haendi shule," Mwangi alisema.

Aliongeza kuwa mamake Wendy alikuwa ametumia fedha hizo kukata kiu chake.

"Ulevi ni kitu kibaya, mamake ni mlevi na amekuwa akiharibu pesa," alisema.

Joe Mwangi aliongeza kuwa ilibidi Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati ili Wendy aweze kupata karo ya shule.

"Ilibidi nimetumia buda... Rais Uhuru mwenye... nikamwambia vile hali iko kuhusiana na fee ya huyu mtoi," Mwangi alisema.

Aliongewa kuwa ni ujumbe wake kwa rais ambapo mtoto huyo aliweza kulipiwa karo na hivyo akaendelea na masomo.

"Baada ya kutumia rais ujumbe, Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i alipiga simu shuleni na kuahidi kulipa karo ya Wendy. Serikali ilimlipia shilingi 53, 000," alisema.

Joe Mwangi alisema kwa sasa anataka kusafisha jina lake kwani yote ambayo yamesemwa na msichana huyo kumhusu si kweli.

"Nataka ukweli ujitokeze na watu wanihukumu kulingana na ukweli," alisema

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...