This archive report was first published on 13 August 2019.
Supkem, chama cha muungano wa Waislamu, kimefutilia mbali leseni ya agenti wa usafiri ambaye anahudumu jijini Nairobi baada ya kudaiwa kuwalaghai waumini wa Kiislamu Ksh 12 milioni walizonuia kutumia kama nauli ya kuelekea Mecca.
Waumini hao walikuwa awamepanga kuhudhuria Hajj ya 2019 huko Saudi Arabia lakini walipigwa na butwaa mtaani Eastleigh, Nairobi baada ya kubaini jamaa aliyekuwa akiwashughulikia katika safari hiyo ametoweka.
Waathiriwa wa kisa hicho walikuwa na gadhabu na wakapiga ripoti katika kituo cha polisi cha Pangani huku baadhi yao wakielekea katika makao makuu ya makosa ya jinai kuandikisha taarifa ila walitumwa katika afisi za DCI za eneo la Starehe.
Supkem ilifichua kwamba Abdi na kampuni yake walikuwa wamejisajili kama biashara halali ila mshukiwa hakutoa orodha ya majina, malipo na pasipoti za wasafiri hao wa 2019 Hajj.
Supkem ilisema, "Muungano huu unakilaani kitendo hicho hususan kutoka kwa maagenti kama vile Abdi, hatua kali zitachukuliwa iwapo kisa kama hiki kitashuhudiwa tena."
Published on August 13, 2019.