This archive report was first published on 13 August 2019.
Kituo cha Thagichu, kaunti ya Tharaka, kilikuwa kwenye kikwazo baada ya mwanadada kukosa kutoa mahari ya mtungi wa asali aliyoagizwa na wazazi wake.
Wazazi walipewa orodha ya vitu vilivyohitajika kama mahari, lakini walisisitiza kwamba aitafute asali kwa udi na uvumba.
Aliposhindwa kuipata asali, alituma wazee kuwapelekea wakwe zake kile achofanikiwa kupata, kwa mujibu wa Taifa Leo.
Alipigwa na butwaa kupokea msomo kutoka kwa wazazi wake, ambao walimtaka kuwa mwangalifu na kujitahidi iwapo aliaka mke.
Wazee walionya, "Kijana usijaribu kutufundisha kukaidi mila. Tuliwaitisha mtungi wa asali ma wala hatuna haja ya pesa zako. Jifunze heshima na kuhifadhi mila mila iwapo unataka tuwe wakwe zako,".
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.