Mwanamke 'amtoka' mumewe baada ya kuvunja vyombo akiwa mlevi ▷ Kenya News

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 13 August 2019.

Kiteta, Mbooni, Kenya - Mwanamke alimtoka nyumbani baada ya kumvunja vyombo vyake akiwa mlevi. Hii ilikuwa baada ya kalameni alivyokuwa akiinywa pombe kupindukia na aliishi kumpuuza mkewe kila apokuwa akimuonya dhidi ya tabia yake.

Alipofika nyumbani, jamaa alifika chakari na kufululiza hadi jikoni. Kwa bahati mbaya, akiwa huko, aliangukia meza iliyokuwa na vikombe na sahani na kuvivunja nyote.

Alipovunja vyombo, mama alikuwa na ujumbe wa kutosha. "Yaani, umeleta ulevi jikoni. Ona sasa matokeo ya ulevi. Kwa nini unavunja vyombo vyangu? Nilikuambia uache pombe lakini ukakataa. Leo sitavumilia. Umenitesa kwa muda mrefu. Pombe utaacha," mama aliwaka huku akisanya vyake na kuondoka.

Penyenye zinaarifu kwamba, mama hakumpa kalameni nafasi ya kujitetea. Kalameni aliachwa mataani huku akigubikwa na machozi akijutia tabia yake.

Published on August 13, 2019 by Tuko.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...