This archive report was first published on 11 August 2019.
Habari 10 Zilizotamba Sana Wiki Hii ¶
Wiki hii ilikuwa na habari nyingi zinazotamba sana nchini Kenya. Kuanzia na shughuli za bunge la Kmaunti ya Homa Bay, ambazo zilisimama kwa muda baada ya mmoja wa MCA kusawazisha hewa kwa mshuto uliotikisa jumba zima.
Waheshimiwa hao walilazimika kuondoka jumbani ili kupunga hewa safi kwani mashuzi ya mmoja wao yalikuwa yenye harufu mbaya mno.
Uzuri wa wiki hii uliendelea na mzozo wa uongozi kati ya kanisa la Nairobi Central SDA (Maxwell Church) na makundi mengine, ambao uliacha waumini wakifungiwa nje ya eneo hilo na kuagizwa kufanya ibada yao katika shule ya upili ya St Georges.
Maafisa wa polisi walikuwa wamezingira kila kona katika kanisa hilo huku waumini waliokuwa wamefika kuhudhuria ibada ya Jumamosi, Agosti 10 wakisalia nje.
Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i amelazimika kubadili kanisa baada ya kanisa sabato tawi la Nairobi Central SDA (Maxwell Church) kukumbwa na mzozo wa uongozi.
Uzuri wa wiki hii uliendelea na kampuni ya kucheza kamari ya Sportpesa, ambayo ilitangaza kuwa imefutilia mbali ufadhili wake kwa vilabu vya spoti mara moja.
Serikali ya kaunti ya Nairobi inatayarisha mswada ambao iwapo utapasishwa basi kuku, mifugo na vile vile mbwa na paka ambao watasafirishwa hadi jijini watatozwa ada ili kuinua ukusanyaji wa ushuru.
Aliyekuwa Mbunge wa Gatundu Kaskazini Clement Waibara, alimkashifu afisa mmoja wa trafiki kwa kumshambulia wakati akimuomba kumuelekeza katika Hospitali Kuu ya Kenyatta.
Wiki hii ilikuwa na habari nyingi zinazotamba sana nchini Kenya.