Arsenal: Mesut Ozil na Sead Kolasinac Wabanduliwa Kikosini Kwa Sababu za Usalama

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 11 August 2019.

Mei 31, 2019

Wachezaji nyota wa Arsenal, Mesut Ozil na Sead Kolasinac, wamebainishwa kushiriki mechi ya ufunguzi ya klabu hiyo ya Ligi Kuu dhidi ya Newcastle kwa sababu za usalama.

Wawili hao walikuwa waathiriwa wa jaribio la kuibiwa gari jijini London kaskazini mwezi uliopita.

Wachezaji hao walishambuliwa jijini London kwa kisu na genge la majambazi katika jaribio la kumwibia Ozil gari lake aina ya Mercedes.

Maafisa wa usalama wa Arsenal wameendelea na uchunguzi wa usalama wao baada ya kisa hicho.

Wachezaji hao walikuwa wakipigana na genge hilo waliokuwa wakijaribu kufikia gari la Ozil kisha wawili hao wakatoroka bila kujeruhiwa.

“Mesut Ozil na Sead Kolasinac hawatakuwa kwenye kikosi chetu cha mechi ya ufunguzi dhidi ya Newcastle United kufuatia visa vya usalama ambavyo bado vinachunguzwa na polisi,” ilisoma taarifa hiyo.

“Tunapania kuwakaribisha wachezaji wetu kikosini,” ilisoma taarifa kutoka kwa klabu hiyo.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...