DP Ruto Awafurusha Wanahabari Kutoka Mkutano Wake

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 11 August 2019.

Naibu Rais William Ruto alikuwa akihudhuria harusi ya kitamaduni ya mwanaharakati Amos Olempaka huko Baringo, Jumamosi, Agosti 10, 2019.

Alipofika, Ruto alisema hakuwa amefika kuongea na wanahabari, bali alikuwa hapo kuzungumza na wakazi.

Maafisa wake wa usalama waliwafurusha wanahabari wote waliokuwepo huku wakiwatoa kwa kasi.

Sherehe hiyo ya harusi ya kitamaduni ya Olempaka ilikuwa inafanywa kulingana na mila na desturi za jamii ya Ichamus huku mamia ya wakazi pamoja na viongozi wakiwa wamehudhuria.

Shambulizi hilo dhidi ya wanahabari lilijiri huku Kenya ikiwa imeratibiwa nambari 100 katika uhuru wa vyombo vya habari ndani ya mataifa 180.

Maafisa wa DP William Ruto waliwafurusha wanahabari kwenye mkutano wake huko Baringo Jumamosi, Agosti 10, 2019. Picha: Lex Ande

Maafisa hao walionekana wakiwabeba wanahabri kihobelahobela na kuwatoa kwenye sherehe hiyo.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...