Dereva na Kondakta wa Basi Linalohusika katika Kifo cha Abiria Wawili Wakamatwa

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 11 August 2019.

Dereva na Kondakta wa Basi Linalohusika katika Kifo cha Abiria Wawili Wakamatwa

Ofisi ya Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai (DCI) imesema, Naphtali Fondo na Alex Gikonyo, wanaazuiliwa kufuatia kifo cha Gerald Kimondo, mwanafunzi wa chuo cha NIBS, aliyekuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Ruaraka Uhai Neema.

Wawili hao watazamiwa kushtakiwa kwa kosa la mauaji wiki ijayo.

Wasiwasi huu unatokana na kifo cha Gerald Kimondo, mwanafunzi wa chuo cha NIBS, aliyekuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Ruaraka Uhai Neema, baada ya kusukumwa nje ya basi lililoenda karibu na Hoteli ya Safari Park mwezi Juni mwaka uliopita.

Aliangukia kichwa kwenye lami na akapata majeraha mabaya sana. Kinya aliaga dunia alipokuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Ruaraka Uhai Neema iliyopo mkabala na alipoangukia.

Ofisi ya DCI ilisema kupitia Twitter, "Dereva na kondakta wa Gari Nambari KCC O21A wamekamatwa kufuatia kifo cha Gerald KIMONDO aliyekuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao; Naphtali FONDO, 33 & Alex GIKONYO, 20, walimsukuma marehemu nje ya basi lililokuwa likienda na kusababisha kifo chake. Watashtakiwa kwa MAUAJI,".

Uchunguzi wa mwanzo uliofanywa na makachero wa @DCI_Kenya wanaoichunguza kesi hiyo umebaini kuwa asi lililohusika pia lilihuska katika kisa sawa na hicho mwaka uliopita (2018) karibu na Hoteli ya Safari Park ambapo Doreen KINYA mwenye umri wa miaka 20 mwanafunzi wa #NIBS alisukumwa nje ya gari na AKAFA.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...