Nairobi: Watu 22 kati ya 300 waliopimwa wapatikana na saratani

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

Primary source Kenyan Digest archive

This archive report was first published on 10 August 2019.

Nairobi: Watu 22 kati ya 300 waliopimwa wapatikana na saratani

Shughuli ya kupimwa ugonjwa wa saratani ilifanyika kwa siku tano kwenye hospitali za Mama Lucy na Mbagathi jijini Nairobi, huku wakazi wa jiji huo wakijitokeza kwa kujisikia na kujitokeza.

Watu 22 kati ya 300 waliopimwa katika hospitali hizo walipatikana kuugua saratani, kwa kujumuisha kina mama na wanawake wengine walio na njia ya uzazi.

Alhamisi, Gavana wa Kaunti ya Nairobi Mike Sonko aliwashukuru wakazi kwa kujitokeza kwenye shughuli hiyo, akisema kuwa waliopatikana na saratani wataendelea kupata matibabu.

"Watu ambao walijitokeza kupimwa ni dhihirisho kamili kuwa tuko tayari kukabiliana na janga la saratani," alisema Sonko.

Uhamasisho wa saratani utazinduliwa rasmi na Gavana Sonko, na utaangazia mitindo ya maisha ambayo wengi wanaishi.

Uzito sasa umewekwa na viongozi kuhusu saratani baada ya viongozi wakubwa kama vile aliyekuwa gavana wa Bomet Joyce Laboso, mkurugenzi wa Safaricom Bob Collymore na aliyekuwa mbunge wa Kibra Ken Okoth kufa kwa ugonjwa huo.

Next read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim Exposed Over Refusal to Repay Ksh 2 Million Debt as Protest Looms at Talanta Plaza

24 July 2026 · 4 min read

Sports Fund CEO Nuh Ibrahim has been exposed over his refusal to repay a KSh2 million debt to a young businessman, with a peaceful...