This archive report was first published on 9 August 2019.
Kituo cha Habari cha Taifa Leo kinatoa taarifa kwamba mwanadada alijikuta pabaya na kuanza kububujikwa baada ya shuga daddy wake kumtaka aolewe na mwanawe.
Demu na sponsa walikuwa wameishi pamoja kwa muda mrefu, na mwanadada alikuwa akitaka amuoe.
Alidai kwamba tayari alikuwa ana familia yake, na kwa hivyo, hakuwezi kukuoa mwanadada.
"Mimi siwezi kukuoa kwa sababu tayari nina mke na watoto. Ningependa uolewe na mwanangu na nitagharamia kila kitu. Nitakuwa nikikufanyia kila kitu," buda alimwambia mrembo.
Demu alichukizwa na kauli ya buda na akaanza kumkaripia huku akidai kwamba hilo halingewezekana.
"Wewe ni mtu wa sampuli gani? Nimekuwa mpenzi wako kwa muda mrefu na sasa unataka niolewe na mwanao. Una akili timamu wewe? Haiwezekani na haitawezekana," kipusa aliapa huku akitishia kumsema jamaa kwa mkewe na jamii yake nzima.