This archive report was first published on 9 August 2019.
Shughuli za bunge la Homa Bay zilisimama kwa muda baada ya mmoja wa MCA kusawazisha hewa kwa mshuto uliotikisa jumba zima.
Waheshimiwa hao walilazimika kuondoka jumbani ili kupunga hewa safi kwani mashuzi ya mmoja wao yalikuwa yenye harufu mbaya mno.
Uvundo huo ulikuwa mkali na kumlazimisha Spika Edwin Kakach kuingilia kati huku MCA wengine wakijaribu kutafuta mshukiwa.
Kitu kilichotokea kwenye bunge la Homa Bay baada ya mmoja wa MCA kusawazisha hewa kwa mshuto uliotikisa jumba zima.
Spika Edwin Kakach alihitaji kuahirisha vikao kwa dakika kadhaa ili kuwapa viongozi hao muda wa kupata hewa safi na jingo hilo pia kuwa na manthari safi ya kufanya kazi.