This archive report was first published on 8 August 2019.
Maandamano ya akina mama katika Kaunti ya Kiambu yaliendelea Jumatano, Agosti 7, 2019, wakililia haki zao baada ya kukosa kutimiziwa mahitaji yao ya ndoa na waume wao.
Waandamanaji hao waliteta wazee kukosa nguvu za kiume, wakisema wengi wa wanaume huondoka nyumbani saa moja asubuhi kwenda kubugia kinywanji kwenye maeneo yaliyogeuka kuwa mwizi wa mahaba kaunti hiyo.
Maeneo ambayo yameadhirika sana ni Limuru mjini, Nazareth, Ngarariga, Farmers Corner, na Kwambira, kwa pamoja na baadhi ya maeneo mengine.
Aliongoza maandamano hayo Susan Nyambura, ambaye alisema hali ni mbaya sana katika maeneo ya Limuru, ambapo alidai kuna kipusa mmoja ambaye amewateka waume wao kwa kuwauzia pombe kwenye nyumba yake.
"Wakifika kitandani atakuguza alafu akuwacha kama hajakutosheleza. Sasa ata huwa hatutaki watuguze. Lakini tunashangaa tutazaa na kina nani," alisema Nyambura.
Aliongeza kuwa kwa sasa akina mama wana wasiwasi kwani wazee wao wameshindwa kushiriki tendo la ndoa.
Walisema maeneo ambayo yameadhirika sana ni Limuru mjini, Nazareth, Ngarariga, Farmers Corner, Kwambira baadhi ya wengine.
Wakazi hao walimtaka Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati na kuwasaidia kupigana na pombe haramu.