This archive report was first published on 8 August 2019.
Mwanamke Achoshwa na Upweke, Azua Kioja Kupiga Mayowe Mjini Akimsaka Mume ¶
Video iliyosambaa Twitter inaonyesha mwanamke huyo akizunguka mjini akiwaamsha watu waliokuwa wamelala huku akipiga mayowe.
Alisimama katika eneo la kuegesha magari na kuwaarifu watu wote waliokuwepo eneo hilo alikuwa amezidiwa na upweke na kwamba alikuwa akimsaka mchumba.
"Amkeni! Namsaka mchumba! Nina upweke mimi! Nimesimama hapa nje," alisema.
Video hiyo ilisambazwa Twitter huku wengi wakiachwa vinywa wazi na jinsi mwanamke huyo aliyoonesha ujasiri wa kuzua kioja hicho.
Wengi wamekataa kusema kwamba mwanamke huyo alikuwa akijitafutia umaarufu, huku wengine wakihisi kwamba jamii imechangia mambo kama hayo kwa kuwashinikiza watu kutafuta wachumba na kuolewa.