This archive report was first published on 8 August 2019.
August 8, 2019, Likoni, Mombasa - Kalameni amesalia na masikitiko baada ya kupokonywa mpenzi wake na bwenyenye mmoja wa mtaani humo.
Alipigwa na butwa kubaini kwamba aliyemnyakua mpenzi wake ni bwenyenye aliyemfahamu vizuri.
Alipowafungulia roho marafiki zake kuhusu tukio hilo, walimshauri ni vyema awachane na kipusa huyo kwa kuwa hangeweza kushindana na mwenye pesa.
"Usiwaingilie, kama amenyakuliwa achana na yeye. Usishindane, ni kawaida ya wanawake kunaswa na matajiri," rafiki mmoja alimweleza polo.
Alipowasikiza wenzake, jamaa aliwadokeza kwamba licha ya mwanadada kumfyonza hela na kunyakuliwa kwingine hatashindana na aliyemnasa.
"Nimesikia ushauri wenu, amenitumia vibaya sana, kala hela zangu nyingi tu huku nikimtimizia mahitaji yake na mshahara wangu kumpa bila kujali. Kwa kuwa kanisaliti na kuniona sifai, haidhuru Mungu atanilipia," jamaa alisema.